Shirikisho la Soka Brazil (CBF) limechagua kituo kipya cha mazoezi kinachomilikiwa na kampuni ya Red Bull kilichopo jijini New York, Marekani kuwa kambi rasmi ya timu ya taifa ya Brazil kwa ajili ya maandalizi ya Kombe la Dunia 2026.
Uamuzi huo unatajwa kuwa sehemu ya mkakati wa kuhakikisha timu hiyo inapata mazingira bora ya kujiandaa kuelekea michuano hiyo mikubwa itakayofanyika nchini Marekani, Canada na Mexico mwaka 2026. Kituo hicho kina vifaa vya kisasa pamoja na mazingira rafiki kwa mazoezi ya kiwango cha juu.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Kocha mkuu wa Brazil, Carlo Ancelotti, amepongeza hatua hiyo akieleza kuwa itasaidia timu kufanya maandalizi katika mazingira yenye ubora wa hali ya juu kabla ya kuanza kwa mashindano hayo.
Ancelotti alisema kuwa CBF imefanya uamuzi sahihi kwa kuchagua kituo hicho kutokana na ubora wake na uwezo wake wa kutoa kila hitaji muhimu kwa timu ya taifa kipindi chote cha maandalizi na wakati wa mashindano.
“Tuna furaha kubwa kwa uamuzi huu. Kituo hiki ni kipya, cha kisasa na kina mazingira yote bora kwa ajili ya kazi yetu kabla na wakati wa Kombe la Dunia 2026,” alisema Ancelotti akizungumzia maandalizi ya Brazil kuelekea michuano hiyo ya dunia.


