Kocha mkuu wa timu ya taifa ya France, Didier Deschamps ameeleza sababu za kumuacha kiungo wa Real Madrid, Eduardo Camavinga katika kikosi kinachojiandaa kwa michuano ya Kombe la Dunia 2026.
Deschamps amesema Camavinga amekuwa na msimu mgumu kutokana na kukumbwa na majeraha ya mara kwa mara pamoja na kushindwa kupata nafasi kubwa ya kucheza ndani ya kikosi cha Real Madrid.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Anatoka kwenye msimu mgumu ambapo hakucheza sana huku akiwa amekabiliwa na majeraha mengi. Bado ni mdogo na nina maamuzi ya kufanya kuhusu muundo wa orodha yangu,” alisema Deschamps.
Kocha huyo pia alikiri kuwa anaelewa maumivu ambayo mchezaji huyo anayapitia baada ya kukosa nafasi ya kushiriki michuano mikubwa zaidi duniani akiwa katika umri mdogo.
“Hata hivyo, ninaweza kupata picha ya masikitiko aliyonayo,” aliongeza Deschamps huku akisisitiza kuwa ushindani mkubwa wa nafasi pamoja na hali ya afya ya Camavinga ndiyo vilivyochangia uamuzi huo.


