Ghana Waibuka na Ushindi Dhidi ya Panama kwa Bao la Dakika za Mwisho.

Black Stars ya Ghana ilipata ushindi mwembamba wa mabao 1-0 dhidi ya Panama siku ya jana katika mechi ya Kundi L ya Taji la Dunia 2026 iliyochezwa kwenye Uwanja wa Toronto nchini Canada.

Ghana Waibuka na Ushindi Dhidi ya Panama kwa Bao la Dakika za Mwisho.

Kipindi cha kwanza, ambacho Panama walikuwa na ubora mkubwa dhidi ya Black Stars, hakikuzalisha mabao kwa upande wowote. Ghana walipata ugumu mkubwa kumuingiza Antoine Semenyo kwenye mchezo, huku safu ya ulinzi ya Panama ikionekana kuwa ngumu kuvunjika.

Ilikuwa ni Caleb Yirenkyi ambaye aliwaokoa Ghana katika dakika ya 90+5 kwa kufunga bao la ushindi na kuwatumbukiza Panama kwenye majonzi. Pasi sahihi ya Brandon Thomas-Asante baada ya shambulizi la kushtukiza ilimaliziwa vyema na Yirenkyi, na kuipa Black Stars bao muhimu katika dakika za mwisho za mchezo.

Panama walifanya kila juhudi katika dakika za mwisho wakisaka bao la kusawazisha, lakini ulinzi wa Ghana ulisimama imara na kuwanyima nafasi ya kupata pointi yao ya kwanza kwenye Taji la Dunia.

Ghana Waibuka na Ushindi Dhidi ya Panama kwa Bao la Dakika za Mwisho.

Kutokana na ushindi huo, Black Stars wamepanda hadi nafasi ya pili katika Kundi L, huku Panama wakibaki nafasi ya tatu kwenye msimamo wa kundi hilo.

Hivyo kwenye Kundi hilo mpaka sasa Ghana wapo nafasi ya 2, huku kinara akiwa ni Uingereza ambaye naye aliibuka na ushindi dhidi ya Croatia. Je kwenye mechi mbili ambazo zimebaki vijana hao wa Carlos Queiroz wanaweza kumaliza nafasi ipi?. Je nafasi yao kufuzu haua inayofuata ikoje?

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.