Kipa mkongwe wa Bayern Munich, Manuel Neuer anaripotiwa kuwa karibu kurejea katika timu ya taifa ya Germany baada ya mazungumzo ya siri yaliyofanyika kati yake na Kocha Mkuu Julian Nagelsmann kuelekea michuano ijayo ya Kombe la Dunia.
Nagelsmann amemjumuisha Neuer kwenye orodha ya awali ya wachezaji 55 wanaotarajiwa kuanza maandalizi ya mashindano hayo makubwa duniani, hatua inayotafsiriwa kama ishara kubwa ya kurejea kwa nahodha huyo wa zamani wa Ujerumani kwenye soka la kimataifa.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Tumekuwa na mawasiliano mazuri katika siku za karibuni na tunaamini uzoefu wake unaweza kuwa muhimu kwa timu,” kilieleza chanzo cha karibu na benchi la ufundi la Ujerumani kuhusu mazungumzo yaliyomshawishi Neuer kubadili msimamo wake wa awali wa kustaafu.
Neuer, ambaye ni mmoja wa makipa waliofanikiwa zaidi katika historia ya soka la Ujerumani, alikuwa ametangaza kujiondoa kwenye majukumu ya timu ya taifa, lakini sasa anaonekana kuwa tayari kuivaa tena jezi ya taifa hilo kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Dunia.
Iwapo kipa huyo ataingia kwenye kikosi cha mwisho cha Ujerumani, ataweka rekodi ya kushiriki michuano ya tano ya Kombe la Dunia, mafanikio yatakayozidi kuthibitisha hadhi yake kama mmoja wa magwiji wakubwa wa soka duniani.


