Mshambuliaji wa Brazil, Neymar, amesema amepitia kipindi kigumu kutokana na majeraha na maneno ya kukosolewa kuhusu hali yake ya kiafya, lakini sasa anaamini yuko tayari kabisa kurejea kikosini kuelekea Kombe la Dunia.
Neymar, ambaye ni mfungaji bora wa muda wote wa Brazil, hajacheza kwa timu ya taifa tangu mwaka 2023 kutokana na majeraha pamoja na upasuaji wa goti uliomuweka nje kwa zaidi ya mwaka mmoja. Kocha mpya wa Brazil, Carlo Ancelotti, amesisitiza kuwa mchezaji huyo anatakiwa kuwa fiti na kucheza vizuri ili kupata nafasi kwenye kikosi cha Kombe la Dunia.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza baada ya klabu yake ya Santos FC kufungwa mabao 3-0 na Coritiba, Neymar alisema anaendelea kuimarika kadri anavyopata muda wa kucheza.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 34 alisema amefanya kila alichoweza ili kurejea katika kiwango chake bora licha ya kupitia kipindi kigumu cha majeraha na maneno mengi kutoka kwa watu waliokuwa wakitilia shaka hali yake.
“Kimwili najihisi vizuri sana na nimekuwa nikiboresha kiwango changu kila mchezo. Nimefanya kila niwezalo, haikuwa rahisi kabisa. Nimefanya kazi kwa bidii kimya kimya licha ya maneno mengi yaliyokuwa yakisemwa kuhusu mimi,” alisema Neymar.
Katika mchezo huo dhidi ya Coritiba, Neymar pia alionekana kukasirishwa baada ya kutolewa kimakosa uwanjani, tukio lililotokea siku moja kabla ya Ancelotti kutangaza kikosi cha Brazil kitakachoshiriki Kombe la Dunia litakaloanza Juni 11 nchini Marekani, Mexico na Canada.


