Wagonga Nyundo wa Uingereza, West Ham United wameingia kwenye mbio za kuwania saini ya beki wa kulia wa Norwich City, Max Aarons. Timu hii ya England inaungana na timu ya Everton na Tottenham Hotspurs ambazo zote zimeonesha nia za kuwania saini ya nyota huyo.

Aarons ni mchezaji wa Norwich City anayeng’ara sana kwa sasa na klabu hiyo huku akiwa na umri wa miaka 21 tu! Aarons alionekana kuvutia timu hizo kubwa za Uingereza kutokana na kiwango chake kikubwa cha uchezaji hasa akiwa kama beki wa kulia mwenye mbio sana hususan kushambulia.

Norwich City walitaka kumuuza na kuna taarifa zilizoeleza kuwa Everton walikuwa kwenye mazungumzo ya ziada na mchezaji huyo lakini kutokana na timu hiyo kurejea ligi kuu ya EPL, wanaweza wakambakisha mchezaji huyo.

Mwaka jana, Aarons alihitajika na moja ya klabu kubwa Uingereza lakini timu yake hiyo ya Norwich City ilikataa ofa ya kumtoa mchezaji huyo. Na kukawepo na mazungumzo yaliyoeleza kuwa angeondoka mwaka mmoja baadaye yaani mwishoni mwa msimu huu.

Akiwa hapo Max amefanikiwa kucheza michezo 42 na kuhusika kwenye magoli 5 ya timu hiyo. Je, Norwich kumuacha mchezaji huyo aende Everton, West Ham or Tottenham? Tusubiri tuone!


MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

Aarons, Max Aarons Ahitajika na West Ham United, Meridianbet

CHEZA HAPA

11 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa