Mchezaji nyota wa kikosi cha Crystal Palace, Wilfred Zaha, ameamua kusema wazi kuwa yupo tayari kujiunga na vilabu vikubwa panapo majaliwa.

Zaha amekuwa akihusishwa na vilabu mbalimbali tangu alipoonesha ubora wake akiwa Palace ambapo kabla ya kujiunga na klabu hiyo, alikuwa ni mchezaji wa Man United.

Nyota huyu raia wa Ivory Coast, amekuwa ni msaada mkubwa kwenye kikosi cha Palace na lilikuwa ni jambo la kumshangaza kocha wake, Roy Hodgson pale ambapo vilabu vilishindwa kufikia dau la pauni milioni 80 ili kumsajili Wilfred Zaha kwenye madirisha mawili ya usajili yaliyopita.

PSG, AC Milan, Arsenal, Everton na Borussia Dortmund ni miongoni mwa vilabu ambavyo vimekuwa vikitajwa kuiwania sahihi ya mshambuliaji huyu bila ya mafanikio yeyote.

Palace itabaki bila kocha kwa muda mfupi baada ya Roy Hodgson kuachana na timu hiyo wikiendi hii. Zaha amegongelea msumari kwenye safari ya Hodgson ambapo na yeye ameamua kujisogeza kwenye mlango wa kutokea Selhurst Park mwishoni mwa msimu huu.

“Ninadhani bado ninayo nafasi ya kufanya vizuri kwenye vilabu vikubwa, kwasababu ni ndoto zangu kushinda vitu vikubwa. Nina uwezo mkubwa wa kwenda kushinda na watu bora zaidi.

“Kama fursa itatokea, siwezi kuikataa kwasababu ninaamini ninastahili hilo. Ni kitu ambacho nitakuja kuwaonesha watoto wangu na kuwaambia ‘baba yenu niliwahi kushinda hiki’. Wilfred Zaha aliiambia The Face.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

River Plate, River Plate, Enzo Perez Aonesha Uwezo Golini., MeridianbetBASHIRI SASA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa