Beki wa zamani wa klabu ya Fc Barcelona,PSG,Juventus kwasasa anaitumikia klabu ya Pumas kutoka nchini Mexico Davi Alves ameweka rekodi na timu ya taifa ya Brazil baada ya kuitwa kwenye kikosi cha kombe la dunia cha taifa hilo.
Beki huyo mkongwe ambae ameibua mijadala mingi baada ya kuitwa kwenye kikosi hicho kutokana na umri wake mkubwa, Lakini kutokana na umri huo ndio kumemfanya kuweka rekodiya kua mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi kuitwa kwenye kikosi cha taifa hilo kinachoshiriki michuano ya kombe la dunia.Beki Alves anaweka rekodi hiyo akiwa na umri wa miaka 39 huku mchezaji wa mwisho kuitwa kwenye kikosi cha Brazil akiwa na umri mkubwa alikua Djalma Santos kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 1966 ambaye alikua na miaka 37.
Dani Alves anaweka rekodi mpya ambayo inatazamiwa kuchukua mda mrefu sana kama ambavyo ilichukua mda mrefu kwa Djalma Santos kutoka mwaka 1966 inavunjwa mwaka 2022.Ingetokea Dani hakuitwa kwenye kikosi cha Brazil ambacho kinashiriki michuano ya kombe la dunia nchini Qatar basi kulikua na mchezaji mwingine wa kuvunnja rekodi ya Djalma Santos ambae ni beki wa klabu ya Chelsea Thiago Silva mwenye umri wa miaka 38.