Kiungo wa klabu ya Yanga Stefane Aziz Ki amepewa likizo ya muda mfupi na klabu yake baada ya kumaliza shughuli nzito ya kupindua meza nchini Tunisia usiku wa jumatano.

Kiungo huyo ambae alifunga goli pekee katika mchezo wa kombe la shirikisho dhidi ya Club Africain ya Tunisia na kuisaidia Yanga kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho baada ya kusubiri kwa miaka minne.aziz kiKiungo Aziz Ki hajarudi na timu hiyo kutoka Tunisia ambapo imewasili nchini leo hii huku yeye akienda mapumziko ya muda mfupi nchini kwao Burkinafaso. Mchezaji huyo imekua rahisi kupata kutokana na adhabu anayoitumikia ya kufungiwa michezo mitatu ya Ligi kuu ya NBC pamoja na kiungo wa Simba Clautus Chama.aziz kiStefane Aziz Ki mchezaji bora wa ligi kuu ya Ivory Coast msimu uliomalizika amefanikiwa kua midomoni kwa watu siku za hivi karibuni kutokana na magoli ambayo amekua akifunga katika michezo muhimu ikiwemo mchezo wa watani wa jadi na mchezo wa juzi dhidi ya Club Africain liliisaidia Yanga kwenda hatua ya makundi.

AVIATOR

Ulishawahi kuwaza kuwa rubani wa maisha yako!! Kuwa rubani wa mchezo pendwa wa Aviator wa kasino mtandaoni. Aviator bonanza inazidi kutoa michongo ya mkwanja kwenye nyumba ya mabingwa. Unarusha ndege yako na unashinda, kuwa rubani wa kujivunia kwa kuibuka na mkwanja leo.

BONYEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa