Kiungo wa timu ya taifa ya Italia anayekipiga katika klabu ya Inter Milan inayoshiriki ligi kuu nchini Italia Nicolo Barella anaamini ya taifa ya Italia ilistahili kuwepo kwenye michuano ya kombe la dunia baada ya kua bingwa wa ulaya.
Timu ya taifa ya Italia ilishindwa kufuzu kwenye michuano ya kombe la dunia baada ya kutupwa nje na timu ya taifa ya North Macedonia katika mechi za mtoano kwa bao moja kwa bila na kushindwa kuwepo kwenye michuano hiyo kwa mara ya pili mfululizo.Mabingwa hao mara nne walishindwa kufuzu kwenye michuano ya kombe la dunia kwa mara ya pili mfululizo ikiwa walishindwa kufanya hivi pia mwaka 2018 ambapo michuano ya kombe la dunia ilifanyika nchini Urusi.
Kiungo Nicolo Barella akieleza kua hajaangalia hata nusu ya michezo kwenye kombe la dunia kwasababu atajiskia vibaya, Lakini akieleza kua mabingwa wa michuano ya Euro na Copa America wanastahili kuwepo kwenye michuano hiyo.Barella hajatofautiana na kocha wake Roberto Mancini ambaye alizungumza mwezi uliopita kua kila bingwa kutoka bara fulani anastahili kupata tiketi ya kufuzu michuano ya kombe la dunia moja kwa moja.