Beki wa zamani wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Liverpool Jamie Carragher amesema licha ya kutolewa kwenye michuano ya kombe la dunia lakini walikua timu bora.
Timu ya taifa ya Uingereza kana ilitolewa katika hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la dunia na mabingwa watetezi wa kombe hilo na timu ya taifa ya Ufaransa kw akufungwa mabao mawili kwa moja.Licha ya kutolewa kwenye mchezo lakini Carragher anaamini Uingereza ni timu bora ambayo imecheza mechi zake tano kwa ubora mkubwa kuliko tim yeyote kwenye michuano hiyo, Beki huyo mkongwe anaamini hata kwenye mchezo ambao wametolewa walicheza vizuri zaidi kuliko washindi.
Gwiji huyo anasema timu ya taifa ya Uingereza haikwenda kucheza na mabingwa watetezi Ufaransa wakiwa kama timu ya daraja la chini, Lakini walicheza mchezo huo wakiwa kama timu bora na yenye wachezaji wenye ubora wa dunia.Jamie Carragher anasema anaamini kizazi cha timu ya taifa ya Uingereza ni bora kuliko ambacho kimewahi kupita kwenye taifa hilo kutokana na ubora ambao wamekua wakionesha vijana hao wa kocha Gareth Southgate.