Mhakama ya usuruhishi ya michezo “The Court of Arbitration for Sport” (CAS) imetupilia mbali shauri lililopelekwa na shirikisho la mpira la Urusi kupinga maamuzi ya FIFA ya kuwaondoa kwenye mashindano ya kombe la Dunia na mashindano yote yanayondaliwa na shirikisho hilo.
Urusi haitashiriki tena mashindano ya kombe la Dunia mwaka 2022 huu nchini Qatar, na timu zote kutoka Urusi na vilabu havitashiriki mashindano yeyote yanayoandalia na FIFA na UEFA baada ya rufani zote kushindwa kwenye mahakama ya CAS.
“CAS, mahakama ya kimichezo, bado inaendelea kutambua haki za kuzuiwa timu zote za kutoka Urusi na vilabu vyake vyote kushiriki mashindano ya FIFA,” waraka wa CAS uliotolewa leo ijumaa.
Siku ya jumanne CAS walitupilia mbali shauri la Urusi kupinga kuondolewa kwenye mashindano yanaoyandaliwa na UEFA kwa timu za taifa na vilabu vyao vya mpira wa miguu.
Wachezaji wampira wa kutoka nchini Urusi na Belarus wamezuiwa kushiriki mashindano mbalimbali, na wengine wameondolewa kwenye vilabu vyao kutokana na nchi hiyo kuivamia nchi ya ukraine kijeshi na nchi ya Belarus akishiriki kumsaidia Urusi.
SHAOLIN FORTUNES 100 ONJA LADHA YA USHINDI
Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.