Cristiano Ronaldo Awekwa Tena Benchi Mechi Dhidi ya Morocco

Fernando Santos kwa mara nyingine tena ameamua kumwacha Cristiano Ronaldo kwenye benchi.

Ronaldo, mwenye umri wa miaka 37, alitajwa kuwa miongoni mwa wachezaji mbadala wa timu yake ya taifa kwenye mechi kati ya Uswizi ya hatua ya 16 bora mapema wiki hii, huku mbadala wake, Goncalo Ramos, akifunga hat-trick.

 

ronaldo

Santos amechagua safu ya mbele ambayo iliirarua Uswizi kwenye njia yao ya kuibuka na ushindi mnono wa 6-1 na uchezaji ambao wengi wameutaja kuwa bora zaidi wa michuano hiyo kufikia sasa.

Uamuzi huo unaweza kusababisha mzozo zaidi kati ya kocha mkuu na mchezaji wake anayetambulika zaidi baada ya Santos mwenyewe kukiri kuwa fowadi huyo hakufurahishwa na uamuzi wa kutomanzisha dhidi ya Uswizi.

“Kwa hivyo, mazungumzo hayo yalihitajika kufanyika,” Santos alisema baada ya kufichua kwamba alimfahamisha Ronaldo mapema kwamba hataanza. ‘Sifanyi hivyo na wachezaji wote. Lakini yeye ni nahodha.

“Nilifanya mazungumzo na Cristiano Ronaldo. Tulizungumza kuhusu timu ya Ureno lakini mazungumzo pekee niliyokuwa nayo ni kabla ya mechi dhidi ya Uswizi kumweleza kwa nini anaenda kuwa mbadala.

 

ronaldo

“Nilimwambia kwamba hataanza katika Raundi ya 16. Hakufurahishwa na mazungumzo hayo, kama ilivyo kawaida. Lakini yalikuwa mazungumzo ya kawaida ambapo kila mtu alionesha mtazamo wake.

“Mchezaji anapokuwa nahodha wa Ureno na kuanza kwenye benchi, ni kawaida kwake kutokuwa na furaha. Nilipomwambia kwamba sitacheza kama nyota, aliniuliza ikiwa ni wazo zuri.

“Bila shaka hakuwa na furaha. Lakini ninakuhakikishia kwamba hakutaka kamwe kuondoka.’

Uamuzi wa kumuacha mchezaji huyo ulifuatia ukosoaji wa Santos dhidi yake kwa majibu yake baada ya kuondolewa dhidi ya Korea Kusini.

Acha ujumbe