Beki wa timu ya taifa ya Brazil na mchezaji wa zamani wa vilabu vya Barcelona, juventus, PSG na klabu ya Sevilla Dani Alves amemsifu kocha wake wa timu ya taifa ya Brazil Adenor Leanardo Bacchi maarufu kama Tite.
Beki Dani Alves ambaye ameweka rekodi ya kua mchezaji taifa hilo kucheza akiwa na umri mkubwa zaidi kwenye michuano ya kombe la dunia akiwa na umri wa miaka 39. Amemsifu kocha wa timu hiyo Tite kwa kufanikiwa kuwapa nafasi wachezaji wote kwenye timu hiyo.Tite kocha wa timu ya taifa ya Brazil amepata sifa kutoka kwa mkongwe huyo baada ya kuhakikisha anawapatia nafasi ya kucheza wachezaji wote 26 walioitw kwenye kikosi cha Brazil mpaka kufikia mchezo wa jana wa hatua ya 16 bora dhidi ya Korea Kusini.
Beki Dani Alves anaamini kocha Tite ni kocha bora ambaye amewahi kumfundisha baada ya kutoa nafasi kwa kila mchezaji wa timu hiyo kuweza kuweka historia ya kucheza michuano hiyo ambayo ni ndoto ya kila mchezaji.Mpaka kufikia katika mchezo wa jana wa 16 bora dhidi ya Korea Kusini wachezaji 25 kati 26 walikua tayari wameshapata dakika za kucheza, Lakini katika mchezo wa jana mwalimu Tite alikamilisha idaidi ya wachezaji 26 baada ya kumtoa kipa Allison Becker na kumuingiza kipa chaguo la tatu Weeverton.