Hatma ya kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamps ipo mikononi mwake mwenyewe pale atapokutana na Rais wa shirikisho la soka nchini humo (FFF) wiki ijayo.
Kocha Deschamps ambaye amefanikiwa kuipeleka timu ya taifa ya Ufaransa kwenye fainali ya kombe la dunia kwa mara ya pili mfululizo, Huku mara moja akifanikiwa kutwaa ubingwa mwaka 2018 na fainali ya mwaka 2022 wakipoteza mbele ya Argentina.Kocha huyo mkataba wake ulikua unamalizika baada ya michuano ya kombe la dunia mwaka 2022, Lakini kocha huyo ana uwezo wa kuendelea kukifundisha kikosi hicho kama atahitaji kwani hatma yangu ipo mikononi mwake.
Rais wa shirikisho nchini humo Noel le Graet amesema kocha Deschamps amefanya kazi nzuri sana na bado yeye ni kipaumbele, Huku akiweka wazi kama kocha huyo atahitaji kuendelea kubaki basi watampa nafasi hiyo.Rais huyo amesema watakua na mazungumzo marefu kidogo kama kocha huyo atahitahji kusalia ndani ya timu hiyo, Lakini ametanabaisha kua mazungumzo yatakua mafupi kama kocha huyo ataamua kuachana na timu hiyo.