Gvardiol Aukubali Mziki wa Messi

Beki wa timu ya taifa ya Croatia Josko Gvardiol ameonekana kukubali mziki wa nahodha wa Argentina baada ya kukutana katika mchezo wa nusu fainali wa kombe la dunia.

Messi ambae ameuwasha moto kwelikweli kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka huu nchini Qatar mpaka sasa akiwa tayari amefunga mabao matano na pasi tatu za mabao, Hivo kumfanya kua mchezaji mwenye mchango mkubwa wa mabao kwenye michuano hiyo.gvardiolBeki kitasa Josko Gvardiol ambaye alikua amecheza kwenye kiwango bora sana kwenye michuano hiyo mpaka alipokutana na Lionel Messi ndipo hali ilibadilika, Kwani beki huyo alikutana na wakati mgumu kwani katika mchezo huo alijikuta akipitia wakati mgumu na Messi akifanikiwa kufunga bao moja na kupiga pasi moja ya bao.

Lakini beki huyo anayekipiga klabu ya Rb Leipzig anaonekana kukubali moto wa Messi kwani beki huyo ameeleza mchezaji huyo anacheza tofauti kidogo na ukilinganisha na klabu yake, Hivo beki huyo amekiri kukutana na Messi mkali sana kwenye michuano hiyo.gvardiolBeki Josko Gvardiol pia anasema anajivunia kucheza na mchezaji bora kwenye historia ya mpira wa miguu, Na kueleza kua siku moja atakaa na watoto wake na kuwaeleza kua alishawahi kucheza dhidi ya mchezaji bora kwenye historia.

Acha ujumbe