Mchezaji wa Real Madrid Eden Hazard amesema kuwa timu yake ya Taifa ya Ubelgiji lazima inyanyue taji kubwa la Kombe la Dunia ikiwa wanataka kuhalalisha lebo ya “Kizazi cha Dhahabu” ambayo wamebeba kwa karibu muongo mmoja.

 

Hazard Asisitiza Ubelgiji Lazima Inyakue Kombe La Dunia.

Ubelgiji inajivunia kikosi cha wachezaji wanaowakilisha baadhi ya klabu kubwa barani Ulaya, wakiwemo Hazard, Romelu Lukaku, Kevin De Bruyne na Thibaut Courtois.

Ubelgiji wamemaliza wa tano  katika miaka saba iliyopita wakiwa kileleni mwa viwango vya FIFA, lakini wameyumba kidogo kuleta matokeo yanayovutia. Ubelgiji waliondolewa katika hatua ya robo fainali ya Mashindano mawili ya Europe  yaliyopita na pia wakatolewa katika hatua hiyo ya Kombe la Dunia la mwaka 2014.

Ubelgiji walifanya vizuri zaidi kwa kutinga nusu fainali ya Kombe la Dunia  Urusi 2018, ambapo walifungwa na Ufaransa, na Hazard anasema lengo la Kombe la Dunia la Qatar ni kusonga mbele.

Hazard aliiambia tovuti rasmi ya FIFA kuwa; “Siku zote kunazungumzwa kuhusu ‘Kizazi cha Dhahabu’ lakini kuna ukweli ndani yake, tumetumia takriban miaka 10 pamoja. Sasa tuna wachezaji wachanga wanaoanza kujitokeza”.

Hazard Asisitiza Ubelgiji Lazima Inyakue Kombe La Dunia.

Hazard aliongeza kwa kusema kuwa wana kizazi cha dhahabu katika timu yao lakini bado hawajashinda chochote na ikiwa wanataka sana kupewa jina hilo la kizazi cha Dhahabu wanahitaji kuongeza jitihada.

Uzoefu wao kwa pamoja umewasaidia katika mashindano yaliyopita kwahiyo anatumaini kuwa wataendelea na hali hiyo kwani muda bado. Hazard ameichezea Ubelgiji mara 122, akimuweka nyuma Toby Alderweireld (123), Axel Witsel (126) na Jan Vertonghen (141) kama mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi nchini mwake.

Mshambuliaji  huyo wa Madrid alifunga mabao matatu katika mechi sita alizochezea Ubelgiji katika Kombe la Dunia la hivi majuzi na anatumai kufanya idadi hiyo kuwa bora nchini Qatar.

Hazard Asisitiza Ubelgiji Lazima Inyakue Kombe La Dunia.

Eden amesema kuwa lazima aweke kiwango chake juu na atajaribu kufanya vizuri zaidi kuliko mwaka 2018 na itakuwa ngumu kwasababu kila timu imejiaandaa na pia hakusita kusema kuwa yeye ana bahati ya kuwa nahodha Taifa hilo kubwa la kandanda na wana deni kwasababu wanatarajia makubwa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa