Nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza Harry Kane ameeleza wanaelekea kwenye mchezo wao wa robo fainali wa michuano ya kombe la dunia dhidi ya mabingwa watetezi Ufaransa siku ya kesho wakiwa na imani zaidi kuliko mwaka 2018.
Uingereza ambao wanatarajia kucheza na Ufaransa kesho kupitia nahodha wao Harry Kane ameeleza kua wanaingia kucheza na timu hiyo wakiwa na matumaini makubwa zaidi kuliko michuano iliyomalizika ambapo wanaamini wataitupa Ufaransa nje ya michuano hiyo hapo kesho.Timu ya taifa ya Uingereza ni miongoni mwa timu ambazo zinapewa nafasi kubwa kuchukua kombe la dunia mwaka na hii ni kutokana na ubora wa kikosi chao na muendelezo bora wa matokeo kwenye michuano mikubwa miaka ya hivi karibuni.
Uingereza wamefanikiwa kuingia fainali ya michuano ya Euro mwaka 2020 huku wakifanikiwa kuingia nusu fainali ya michuano ya kombe la dunia iliyofanyika nchini Urusi mwaka 2018, Hivo hii inaonesha kwanini timu hiyo inapewa nafasi kubeba taji hilo.Harry Kane amekiri anajua mchezo wa kesho ni mgumu sana kwao lakini watahakikisha wanapambana kushinda mchezo huo kwani hawapo kushinda mchezo wa robo fainali tu, Anaeleza timu hiyo imejiandaa kufanya makubwa zaidi mwaka huu kutoka na imani yao kua juu zaidi.