Wakala wa kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp amefuta uwezekano wa kocha huyo kuchukua nafasi ya kocha wa sasa wa timu ya taifa ya Ujerumani Hans Flick baada ya kocha huyo kushindwa kuivusha timu hiyo hatua ya mtoano.

Ujerumani chini ya Hans Flick imefanikiwa kushinda mchezo mmoja huku wakifungwa mmoja na kusuluhu mmoja hivo kuwafanya kua na alama nne sawa na timu ya taifa ya Hispania huku wao wakitoka ka tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa.kloppTimu ya taifa ya Ujerumani wanatoka kwenye hatua ya makundi kwa mara ya pili mfululizo baada ya kutolewa kwenye michuano hii mwaka 2018 yalipofanyika nchini Urusi na mwaka huu kujirudia tena na hii inaonesha kuna kila dalili Flick akaondoshwa kwenye timu hiyo.

Kwa wakati huu ambao timu ya taifa ya Ujerumani imefanya vibaya huku mjadala mzito ukiibuka kuhusu kufaa kwa kocha Flick,Huku Klopp na Tuchel wakihusishwa kwa karibu kuchukua nafasi ya Flick.kloppWakala wa kocha Klopp yeye ameeleza kua mteja wake hatapendezwa kuchukua jukumu la kufundisha timu ya taifa ya Ujerumani na kusema huo ni mjadala wa vyombo vya habari huku akisema kocha huyo ana mkataba mpaka 2026 ndani ya Liverpool na ana mpango wa kuukamilisha.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa