Kocha wa timu ya taifa ya Croatia Zlatko Dalic amesema yeye hakerwi na aina ya ushangiliaji  wa wachezaji wa timu ya taifa ya pale wanapokua wamefunga bao katika mchezo.

Siku za hivi karibuni kumekua na mapingamizi kutoka kwa wachambuzi wa mpira pamoja wa wadau mbalimbali wa soka ikiwemo gwiji wa zamani wa klabu ya Manchester United Roy Keane, Kua aina hiyo ya ushangiliaji ya timu ambao hucheza kila wanapofunga bao inakua kama kuikosea heshima timu timu pinzani.kochaDalic yeye ameweka wazi hakerwi na aina hiyo ya ushangiliaji kwasababu huo ni utamaduni wao hivo wana haki ya kufanya hivo na hiyo haioneshi kumkosea heshima mtu yeyote kama ambavyo wengine wanatafsiri.

Kocha huyo amefunguka hayo wakati wa kuelekea mchezo wao wa robo fainali kati ya timu yake dhidi ya timu ya taifa ya Brazil ambapo pia ameeleza kua hatafurahishwa kuona wachezaji wake wanashangilia kama hivo kwakua sio utamaduni wao.kochaKocha Dalic amefunguka kua ni kitu kizuri kucheza dhidi ya taifa ya Brazil kwasababu kila timu ingekua na ndoto hiyo, Na kueleza kua Croatia imekua ndani ya timu nane bora mpaka sasa na wanataka kufanya vizuri zaidi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa