Kocha wa wa timu ya taifa Croatia Zlatko Dalic amesema hawana haja ya kumuhofia nahodha wa timu ya taifa ya Argentina Lionel Messi kama watatumia mbinu walizotumia kumzuai staa wa timu ya taifa ya Brazil Neymar.
Timu ya taifa ya Croatia itakutana na timu ya taifa ya Argentina kwenye nusu fainali ya kombe la dunia baada ya kuitupa nje timu ya taifa ya Brazil hapo jana kupitia mikwaju ya penati baada ya mchezo kumalizika kwa suluhu.Kocha Dalic anaamini kama watarudia ambacho wamekifanya dhidi ya timu ya taifa ya Brazil basi wana uhakika wanaweza kumtuliza mchezaji huyo kwani wanajua ubora wake, Lakini watahakikisha wanamdhibiti nyota huyo kama ambavyo walifanya dhidi ya Neymar.
Dalic anatambua fika kua Messi ni mchezaji hatari na ndio anaibeba timu ya taifa ya Argentina lakini anaelewa pia timu hiyo ina vijana wadogo wenye uwezo mkubwa na hatari pia, Lakini kocha huyo amesisitiza watajitahidi kutoa ubora wao kwa aslimia mia moja ili kuweza kupata matokeo katika mchezo huo wa nusu fainali utakaopigwa siku ya jumanne.Timu ya taifa ya Argentina imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuitupa nje timu ya taifa ya Uholanzi kwenye mikwaju ya penati usiku wa jana baada ya kumaliza dakika 120 kwa suluhu ya mabao mawili kwa mawili.