Kocha Morocco: Makocha wa Kiarabu Wanastahili Nafasi Klabu Kubwa

Kocha wa timu ya taifa ya Morocco Walid Regragui anaamini makocha wa kiarabu wanastahili nafasi katika timu kubwa, Hii ni baada ya timu ya tafa ya Morocco kufanikiwa kuitupa nje timu ya taifa ya Hispania kwenye michuano ya kombe la dunia.

Kocha huyo ambaye alichaguliwa kuifundisha timu hiyo mwezi wa nane mwaka huu baada ya kuondolewa kwa aliekua kocha wa timu hiyo Handinovic. Walid amefanikiwa kumaliza hatua ya makundi akiwa maeruhusu bao moja pekee dhidi ya Canada na kumaliza wakiongoza kundi mbele ya vigogo kama Ubelgiji na timu ya taifa ya Croatia.kochaWalid amefanikiwa kuiongoza timu ya taifa ya Morocco kua timu ya kwanza ya kiarabu kufika robo fainali ya kombe la dunia ikiwa ni historia kwa taifa hilo na nchi za kiarabu kwa ujumla na kumfanya kocha huyo kuamini wanaweza kupata nafasi sasa kwenye vilabu ikubwa kwasasa.

Walid alipoulizwa kwanini timu kubwa hazichukui makocha wa kiarabu yeye akijibu labda ni utamaduni ambao wamejiweka lakini kwasasa makocha kutoka nchi za kiarabu wanaweza kuchukua nafasi katika vilabu kama Manchester City au Barcelona.kochaKocha Walid Regragui anasema amekua akifanya kazi ya ukocha kwa miaka 10 sasa lakini hakuna aliekua anamtazama kwasasa yupo robo fainali ya michuano ya kombe la dunia ikiwa ni maajabu makubwa ambayo hakuna alietarajia.

Timu ya taifa ya Morocco inatarajiwa kucheza mchezo wake wa robo fainali dhidi ya timu ya taifa ya Ureno kwenye michuano ya kombe la dunia siku ya jumamosi, Ukirajiwa kua mchezo mkali na wenye mvuto mkubwa.

 

Acha ujumbe