Kocha wa timu ya taifa ya Hispania Luis Enrique amezungumza na kuomba radhi baada ya kutangaza kuachana na timu hiyo siku ya leo punde tu baada ya kutupwa nje kwenye michuano ya kombe la dunia.

Hispania ilicheza na timu ya taifa ya Morocco siku ya Jumanne na mchezo huo kwenda hadi dakika 120 bila bao kwa timu yeyote na hatimae Hispania kutupwa nje kwenye michuano hiyo kwa mikwaju ya penati.luis enriqueLuis Enrique ambaye amedumu na timu hiyo kwa takribani miaka minne akiwa pia amepata mafanikio kadhaa kama kufika hatua ya fainali  kwenye michuano ya Uefa Nations League mara kadhaa pamoja na kuingia nusu fainali ya michuano ya Euro mwaka 2020.

Kocha huyo ameweza kuushukuru uongozi wa soka nchini Hispania ambao ulimpa nafasi kwenye timu hiyo mwaka 2018, Lakini ameweza kuomba radhi kwa kitendo chake cha kuachana na timu hiyo wakati ambao amlishindwa kuisaidia kupata mafanikio zaidi lakini hana budi kuangalia maisha mengine.luis enriqueMwisho kabisa Luis Enrique amaeweza kuwashukuru wachezaji wake ambao amekua akifanya nao kazi kwa kipindi chote alichoitumikia timu hiyo, Bila kusahau mashabiki wa timu hiyo ambao wamekua mstari wa mbele kuisapoti timu hiyo.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa