Beki wa timu ya taifa ya Uingereza na klabu ya Manchester United Harry Maguire anaamini nyota mwezake wa kikosi hicho Marcus Rashford anaweza kua miongoni mwa wachezaji bora duniani.

Marcus Rashford alipoteza nafasi kwenye kikosi cha Southgate baada ya kua na msimu mbovu mwaka 2021/22 na kufanikiwa kufunga mabao manne tu msimu mzima jambo ambalo linaonesha ubora wake umeshuka.maguireLakini Rashford amekua na msimu bora sana chini ya mwalimu Ten Haag baada ya tayari kufunga mabao nane kwenye michuano yote msimu huu na kulazimisha kurudi kwenye kikosi cha mwalimu Gareth Southgate.

Rashford ambaye alifunga mabao mawili katika mchezo wa mwisho wa kundi dhidi ya Wales katika ushindi wa mabao matatu kwa bila Uingereza walioupata kwenye mchezo huo na Rashford kufikisha mabao matatu sawa na Alvaro Moratta, pamoja na Kylian Mbappe.

Maguire alipoulizwa kuhusu kiwango cha Rashford alisema “Nimefurahishwa sana na Rashford. Sidhani kama atafika uwezo wa kipaji chake, Lakini ninaamini ana talanta kubwa na anaweza kua bora ulimwenguni ni yeye anapaswa kujisukuma na kujitahidi kwenye hilo”maguireMaguire anakiri kwenye kipindi cha mwaka mmoja uliopita Marcus Rashford hakua kwenye kiwango bora na ilimuathiri lakini kwasasa mchezaji huyo anaonesha ubora mkubwa baada ya kurejesha makali yake ya misimu kadhaa nyuma.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa