Kocha kuu wa Italia Roberto Mancini amedokeza kuwa timu yake pendwa Argentina inaweza kushinda Kombe lao la tatu la Dunia huku mchezaji wa PSG Lionel Messi na wachezaji wenzake wakitafuta sifa nzuri nchini Qatar.

Kikosi cha Mancini cha Italia hakitashiriki michuano hii  baada ya kushindwa kwenye mchujo dhidi ya Macedonia Kaskazini kwa bao 1-0 mwezi Machi, huku kukosekana kwa Italia Qatar kunakuja licha ya wao kuwa mabingwa wa michuano ya Eoro baada ya kumtungua Uingereza kwa mikwaju ya penalti kwenye Fainali.manciniUshindi huo baadaye uliwafanya wakabiliane na Argentina katika Fainali ya UEFA/CONMEBOL Uwanja wa Wembley mnamo Juni, baada ya vijana wa Lionel Scaloni kushinda Copa America. Argentina iliishinda Italia 3-0, na Mancini amesema kwamba uchezaji unachangia katika kuwapanga wachezaji wanaopendekezwa kwa Kombe la Dunia.

Mancini alisema kuwa; “Kuna timu nyingi zenye nguvu, ikiwa ningehitaji kuchagua moja, ningeenda Argentina kwani walivutia sana tulipocheza nao”

Italia wameshinda mechi zao tatu zilizopita huku wakitarajia kushinda masikitiko ya Kombe la Dunia kwa kucheza mechi za kirafiki ambapo walishinda dhidi ya Albania kwa 3-1 Jumatano, huku wakijiandaa kucheza mchezo mwingine dhidi ya Austria siku ya leo.manciniMancini bado anasikitishwa na kushindwa kufika Qatar, lakini amefurahishwa na majibu ya timu yake, akisema: “Tulionyesha nia ya kupambana mara moja, kushinda kundi la Ligi ya Mataifa ambayo haikuwa rahisi kwa Ujerumani, Hungary na Ujerumani na wakati ujao watahitaji kuwa bora zaidi.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa