Staa na nahodha wa timu ya taifa ya Argentina anayekipiga katika klabu ya PSG Lionel Messi amemkosoa kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi kutokana na mbinu alizotumia katika mchezo dhidi yao usiku wa jana.
Kocha Louis Van Gaal alizungumza siku moja kabla ya mchezo huo na kusema watamzuia staa huyo kama ambavyo walifanya kwenye kombe la dunia nchini Brazil ambapo alieleza walimfanya Messi kutokua na madhara.Kocha Van Gaal pia alieleza pia watakwenda kucheza kwenye mchezo dhidi ya timu ya taifa ya taifa Argentina katika mchezo wa robo fainali na hapo ndipo staa huyo alipomkosoa kocha huyo baada ya kubadili ambacho alikisema hapo awali.
Nahodha huyo wa Argentina alimkosoa kocha huyo kwa kusema atacheza mpira mzuri dhidi yao lakini mwisho aliishia kuingiza watu warefu ili kucheza mipira ya juu tu, Ikumbukwe kocha Van Gaal aliwaingiza washambuliaji wawili Luke De Jong na Weighorst aliefanikiwa kusawazisha mabao yote mawili.
Timu ya taifa ya Argentina imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuitoa timu ya taifa ya Uholanzi kwa mikwaju ya penati, Hiyo ni baada ya timu ya taifa ya Uholanzi kusawazisha mabao yote mawili ambayo timu ya taifa ya Argentina waliyapata.Mshambuliaji Lionel Messi usiku wa jana alionekana ni mwenye kujawa na hisia zaidi usiku wa jana baada ya kwenda kwenye benchi la Uholanzi na kutoa maneno yasiyo ya kiungwana pamoja na kumtolea maneno mabaya mshambuliaji wa Uholanzi Weighhorst wakati akifanya mahojiano na wanahabari.