Kocha wa timu ya taifa ya Morocco amesema kua atafurahi kama staa wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ataanzia nje kwenye mchezo wa robo fainali wa michuano ya kombe la dunia dhidi ya timu ya Ureno.
Kumekua na maneno mengi kua timu ya taifa ya Ureno inacheza vizuri bila ya nyota huyo huyo ambapo alianzia nje kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora dhidi ya timu ya taifa ya Uswisi na kufanikiwa kushinda kwa mabao sita kwa moja.Kocha wa timu ya taifa ya Morocco anasema licha ya kua Ureno inaonekana kua bora bila ya Ronaldo kama ambavyo watu wanasema lakini kwa upande wake anaona bora staa huyo aendelee kuanzia nje kwenye mchezo dhidi yao, Kwasababu anajua ni miongoni mwa mchezaji bora kwenye historoa ya mpira.
Kocha huyo anaeleza kua kubwa zaidi ambalo wanaliangalia ni kwenda kukabiliana na Ureno ambayo inaonekana ina njaa kubwa na kuhitaji kuingia kwenye vitabu vya historia, Huku akiamini watakua na mashabiki wengi uwanjani hvo wanaweza kufanya jambo.Timu ya taifa ya Morocco wamefanikiwa kuweka historia kwa kufanikiwa kua timu ya kwanza ya kiarabu kuingia hatua ya robo fainali ya kombe la dunia, Pia timu ya nne kutoka Afrika kufanya hivo baada ya Cameron, Senegal, na Ghana.