Staa wa timu ya taifa ya Brazil Neymar Jr amemjia juu wakala wake wa zamani Wagner Ribeiro baada ya kumzungumza vibaya aliyekua kocha wa timu ya taifa ya Brazil Adenor Leonardo Bacchi.
Wakala huyo wa zamani wa Neymar alitumia mtandao wake wa kijamii wa Instagram na kuposti picha ya Tite punde tu baada ya Brazil kutolewa kwenye michuano ya kombe la dunia na kuandika “Mtu huyu hakuwahi kua kocha wa mpira ametumia miaka miwili kuwahadaa watu huku akipoteza vikombe viwili”Kitendo cha wakala huyo kuandika hivo kilimkasirisha staa huyo na kumtaka asiongee upuuzi juu ya kocha huyo, Hii imekuja punde baada ya Brazil kutupwa nje ya michuano na kocha wa Brazil Tite kujiuzulu kuhudumu kwenye timu hiyo.
Baada ya wakala huyo kuongea hivo watu wengi wameonekana kumunga mkono lakini Neymar ambaye aliona ni kumkosea heshima kocha huyo kwani Tite ameshinda mataji kadhaa akiwa na vilabu kama Club Internacional na Corithians vyote vya Brazil pamoja taji la Copa America 2019 akiwa na Brazil.Kocha wa timu ya Brazil alieleza mapema mpango wake kustaafu baada ya michuano ya kombe la dunia mwezi Febuari mwaka huu na sio kweli kama kocha huyo amejiuzulu kwenye timu hiyo baada ya kutolewa kwenye michuano ya kombe la dunia.