Christian Pulisic Awatoa Hofu Mashabiki

Christian Pulisic amewapa nguvu mashabiki wa Marekani na timu yake ya taifa kabla ya mechi yake ya hatua ya 16 bora dhidi ya Uholanzi Jumamosi asubuhi.

 

pulisic

Pulisic alifunga bao la ushindi katika mchezo wao wa mwisho wa kundi dhidi ya Iran na kujihakikishia kusonga mbele, kabla ya kupata jeraha la tumbo ambalo lilitokea wakati wa akifunga baadae alipelekwa hospitali.

Huku kukiwa na hofu juu ya hali yake, kile kinachoonekana kuwa picha kwenye snapchat ya Pulisic akiwa kitandani kwake hospitalini imeibuka kwenye mitandao ya kijamii, iliyotumwa tena na akaunti rasmi ya timu ya Marekani, ikimuonyesha akishangilia.

Soka la Marekani lilifichua baadaye Jumanne kwamba Pulisic alikuwa na mtikisiko wa ‘pelvic’ na ni siku hadi siku lakini tayari alikuwa amejiunga na kikosi kwenye hoteli ya timu wakati waliporejea kutoka kwenye mchezo.

 

pulisic

Picha inayozungumziwa ina maelezo mafupi: “Najivunia ninyi nitakuwa tayari Jumamosi msijali.”

Wanaosubiriwa ni Uholanzi waliomaliza kileleni mwa Kundi A mbele ya Senegal, Ecuador na wenyeji, Qatar.

Pulisic amekuwa akisifiwa na wachezaji wenzake na vyombo vya habari, kwa vile Marekani ilifuzu katika hatua ya mtoano kabla ya robo fainali ya kombe la dunia.

Kocha Gregg Berhalter hakutoa taarifa za kina kuhusu winga huyo wa Chelsea kufuatia ushindi wa timu yake dhidi ya mpinzani wake wa muda mrefu, Iran.

“Hakuna taarifa kuhusu hali yake,” Berhalter alisema kuhusu Pulisic.

“Lakini nimekuwa nikisema muda wote, ni jambo la ajabu wakati mmoja wa wachezaji wako bora ni mmoja wapo wa kazi ngumu zaidi, Siwezi kusema mambo chanya ya kutosha kuhusu Pulisic”.


Je wewe hucheza Kasino Mtandaoni na umekuwa ukijiuliza ni mchezo gani rahisi na mzuri kwa ushindi? Basi Usihangaike Aviator ni rahisi zaidi kucheza na kushinda, kingine cha zaidi ni kwamba Aviator Bonanza imerudi tena Cheza zaidi ujiweke kwenye nafasi ya kushinda Samsung A23.

CHEZA HAPA

 

pulisic

Acha ujumbe