Mashibiki kutoka sehemu mbalimbali za dunia ambao watasafiri kwenda nchini Qatar wa ajiri ya kushuhudia mashindano ya kombe la dunia mwaka hu wataruhusiwa kunywa bia kwenye maeneo ya mashabiki na viwanja vyote.

Sera ya hiyo ya kuruhusu unywaji wa bia imepitishwa na muandazi wa mashindano hayo ambapo asilimia kubwa ya wakazi wa nchini Qatar ni waislam, hivyo mashabiki wawataruhusiwa kunywa bia kabla na baada ya mchezo kumalizika ndani ya viwanja nane.

Qatar, Qatar 2022: Bia Zaruhusiwa kwenye Mashindano ya Kombe la Dunia, Meridianbet

Watoa huduma waliruhisiwa kununua  champagnes, wine, bia na vileo vikalo kama sehemu ya ‘corporate packages’ tangu mwaka 2021.

Kampuni ya AB InBev ambao ni wazalishaji wa bia aina ya Budweiser ndio bia rasmi kwa ajiri ya mashindano ya kombe la dunia tangu mwaka 1986 na mpaka mwaka mwaka huu ndio bia rasmi ya ya msahindano hayo.

Kulingana na FIFA: “Pombe zitauzwa ndani ya viunga vya uwanja kabla ya mechi kuanza na baada ya mechi kuisha”

“Ndani ya uwanja wenye tiketi na vikombe wataweza kupata bia isiyo na kilevu ya Budweiser Zero,” FIFA walisema kwenye waraka huo.

Pia matumizi ya vileo kwenye maeneo ya wazi yamepigwa marufukum, japokuwa hoteli na bar zote zimepewa vibali vya kuuza vileo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa