Kiungo wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya Juventus inayoshiriki ligi kuu nchini Italia Adrien Rabiot amesema timu ya Ufaransa haimtegemei mshambuliaji Kylian Mbappe.

Mshambuliaji Kylian Mbappe mpaka sasa yupo kileleni kwenye orodha ya wafungaji bora wa michuano ya kombe la dunia mwaka baada ya kufunga mabao matano na kupiga pasi mbili za mabao. Mbappe amejipambanua kama mchezaji muhimu wa timu ya taifa ya Ufaransa.rabiotKiungo Rabiot anakiri Mbappe ni silaha yao kubwa kwenye kikosi lakini anaamini kwenye timu hiyo haimtegemei Mbappe tu kupata matokeo kwani kuna wachezaji wengine wenye uwezo wa kuipatia timu hiyo matokeo na kufanya mabadiliko mda wowote.

Rabiot anaeleza wanamuhesabu Mbappe kama wachezaji wengine kwenye kikosi na cha msingi ni kuomba kila mchezaji kwenye timu yao awe fiti kuelekea mchezo wao wa Robo fainali dhidi ya Uingereza.rabiotUfaransa watamenyana na Uingereza katika mchezo wa robo fainali ya kombe la dunia siku ya jumamosi ambapo timu zote mbili ziliofanikiwa ktinga hatua hiyo kwa ushindi wa mabao matatu, Hivo mchezo huo unatarajiwa kua mkali na wenye ushindani mkubwa.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa