Rice Kukipiga dhidi ya Ufaransa

Kiungo wa timu ya taifa ya Uingereza anayekipiga katika klabu ya West Ham Declan Rice yuko fiti kukipiga dhidi ya taifa ya Ufaransa siku ya Jumamosi ameeleza mchezaji mwenzake Kalvin Philips.

Kiungo huyo alikosekana mazoezini siku ya jumatano kutokana na maumivu ambayo hayakuwekwa wazi hivo kuleta taharuki kubwa ka huenda kiungo huyo atakosekana katika mchezo wa robo fainali dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa.ricePhilips ambaye alitengeneza muunganiko bora kabisa na Rice katika michuano ya Euro mwaka 2020 na kuiwezesha timu hiyo kufika fainali ya michuano hiyo ameonesha kutokua na wasiwasi nakiungo mwenzake huyo kuwepo katika mchezo wa robo fainali jumamosi

Declan Rice amekua mhimili na mchezaji wa kutegemewa kwenye safu ya kiungo cha timu ya taifa ya Uingereza chini ya kocha Gareth Southgate kutokana na ubora ambao amekua anauonesha tangu alipoanza kupata nafasi kwenye timu hiyo.riceTimu ya taifa ya Uingereza inatarajiwa kucheza dhidi ya timu ya taifa ya Ufaransa siku ya jumamosi katika mchezo wa robo fainali ya kombe la dunia. Mchezo huo unatarajiwa kua wa kusisimua kutokana na ubora wa timu zote mbili.

Acha ujumbe