Ronaldo Awapiga Dongo Wakosoaji

Staa na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo amewapiga dongo wakosoaji wote ambao wanataka kuharibu hali ya utulivu na umoja katika kambi timu ya taifa ya Ureno kwenye michuano ya kombe la dunia.

Kumekua na ukosoaji mkubwa kwa staa huyo tangu atangaze kuondoka katika klabu ya Manchester United mapema mwezi uliomlizika, Hii imepelekea nyota huyo kuandamwa sana na vyombo vya habari ambapo staa huyo ameona kama ukosoaji huo una lengo baya la kuathiri timu yao ya taifa.ronaldoTangu Ronaldo aondoke klabuni Manchester United na kufanya mahojiano na mwandishi nguli kutoka nchini Uingereza Piers Morgan, Hali ilibadilika ghafla na kuanza kupigwa mawe kwenye kila anachokifanya pamoja na kuripotiwa kua na ugomvi na baadhi ya wachezaji wenzake kama Bruno Fernandes jambo ambalo limekanushwa na mchezaji huyo mwenyewe.

Staa huyo ameposti kwenye mitandao yake ya kijamii siku ya leo na kueleza kua umoja wa timu hiyo hauwezi kuvunjwa na maneno kutoka nje, Ronaldo kama nahodha wa timu hiyo ni jukumu lake kusimama na kuimarisha umoja kwenye timu pale ambapo anapoona unataka kuvurugika kama ambavyo amefanya leo hii.ronaldoTimu ya taifa ya Ureno inatajiwa kucheza mchezo wake wa robo fainali dhidi ya timu ya taifa ya Morocco siku ya jumamosi baada ya kupata ushindi mnono kwenye hatua ya 16 bora dhidi ya Uswisi kwa jumla ya mabao sita kwa moja.

Acha ujumbe