Sanamu iliyokuwa ukimuonesha Zinedine Zidane akimpiga kichwa mchezaji wa Italia Materazi kwenye fainali za kombe la dunia 2006 itarudishwa tena nchini Qatar baada ya kuondolea mwaka 2013 kutokana na kupingwa na wenyeji wa nchi hiyo.

Sanamu hiyo iliyopewa jina la “Coup de tete” iliondolewa siku kadhaa baada ya kutambulishwa  kutokana nwa watu kutoka chama cha conservative Muslim kukosoa kwa kuhamasisha ibada ya masanamu na wengine wakisema kuwa inachochea vurugu.

Qatar

“Mapinduzi yanatokea kwenye jamii, Inachukua muda watu kuelewa  na watakosoa sana mwanzoni, lakini baadae wataelewa na watazoea,”  alisema mwenyekiti wa makumbusho nchini Qatar Sheikha al-Mayassa al-Thani dada wa kiongozi wa nchini humo.

Sheikha al-Mayassa alisema sehemu ambayo iliwekwa hiyo sanamu haikuwa sawa na badala yake ingewekwa kwenye makumbusho ya michezo jijini Doha, ambapo kwa mwaka huu ndipo kunapokwenda kufanyika mashindano ya kombe la dunia.

Baadhi ya wanachama wa conservative Muslims nchini Qatar, wanaamini sanaa ya kuiga umbo au mfano wa binadamu  unapaswa kupigwa marufuku ili kuondoa ibada za masanamu. Ingawa sanamu zipo sehemu nyiingine sana duniani kwenye maeneo ya wazi lakini kwenye ukanda wa uarabuni ni nadra sana kuona.

Al-Mayassa aliwaambia waandishi kuwa kusudi la kuionesha sanamu hiyo mi kufikisha ujumbe  kuhusu “msongo wa mawazo kwa wachezaji” na umuhimu wa kushighulikia tatizo hilo la afya ya akili.


SHINDA SAMSUNG A32 NA AVIATOR

SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!

kasa wa njano, Kasa wa Njano Awapa Ubingwa wa CL Liverpool., Meridianbet

SOMA ZAIDI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa