Santos: Ronaldo Hajataka Kuondoka Ureno

Kocha wa timu ya taifa ya Ureno Fernando Santos ameweka wazi staa wake Cristiano Ronaldo hajaomba kuondoka kwenye kambi ya timu ya taifa ya Ureno huko nchini Qatar ambapo michuano ya kombe la dunia ikiendelea.

Kocha huyo amesema kua staa huyo hajaomba kuondoka kwenye timu hiyo baada ya kuwekwa nje katika mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Uswisi kwenye hatua ya 16 bora, Lakini akiweka wazi kua staa huyo alikasirishwa na kitendo cha kuwekwa nje kwenye mchezo huo.santosKocha Santos pia amewataka watu kuacha kumkosea heshima staa huyo kwani amelitumikia taifa hiko kwa heshima kubwa tangu ameanza kuchezea timu ya taifa ya Ureno na kuwataka mashabiki kumpa heshima yake gwiji huyo.

 

Pia Santos ameeleza alifanya mazungumzo binafsi na staa huyo kwakua ni nahodha wake na hua hafanyi hivo kwa kila mchezaji lakini akiwataka watu kupuuza taarifa za Ronaldo kutaka kuondoka timu ya taifa kwakua hazina ukweli wowote.santosKocha huyo ameyazungumza hayo katika mahojiano dhidi ya waandishi wa habari kuelekea mchezo wao wa robo fainali kwenye michuano ya kombe la dunia hapo kesho dhidi ya timu ya taifa ya Morocco.

Acha ujumbe