Timu ya taifa ya Senegal imeanza kuonesha makali katika michuano yta kombe la dunia nchini Qatar baada ya kuwafunga wenyeji wa michuano hiyo timu ya taifa ya Qatar kwa mabao matatu kwa moja mapema leo.
Vijana wa Alliou Cisse walionekana kua na makali katika vuipindi vyote katika mchezo baada ya kupata bao katika kila kipindi huku kipindi cha kwanza wakifanikiwa kufunga bao moja huku kuoindi cha pili wakipachika mabao mawili na kufanya jumla kua matatu.Mabao ya Boulaye Dia,Famara Diedhiou, pamoja Bamba Dieng yalitosha kuipa alama tatu muhimu Simba wa Teranga huku bao la kufutia machozi la wenyeji likifungwa na Mohammed Muntari alieingia akitokea benchi.
Mpaka sasa timu ya taifa ya Senegal mabingwa watetezi wa kombe la Afrika wamefanikiwa kufikisha alama tatu baada ya kuwafunga Qatar huku wakibakisha mchezo mmoja ili kuweza kukamilisha idadi ya michezo ya makundi, Pia wakihitajika kushinda mchezo huo ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.Senegal inakua timu ya kwanza ya Afrika kupata matokeo ya ushindi kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka huu katika mchezo wake wa pili, Huku timu zingine kutoka Afrika zikiwa bado hazijafanikiwa kupata matokeo ya ushindi.