Newcastle, Bayern Munich Waanza Mazungumzo ya Anthony Gordon

Klabu ya Newcastle United na Bayern Munich zimeripotiwa kuanza mazungumzo rasmi ya klabu kwa klabu kuhusu uwezekano wa kufanikisha usajili wa winga Anthony Gordon katika dirisha lijalo la usajili.

Newcastle, Bayern Munich Waanza Mazungumzo ya Anthony GordonHatma ya Gordon ndani ya Newcastle inaonekana kutokuwa na uhakika mkubwa, huku taarifa zikidai kuwa uwezekano wa nyota huyo kuondoka katika dimba la St James’ Park msimu huu wa kiangazi unaongezeka siku hadi siku.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za usajili Florian Plettenberg, Bayern Munich tayari imeanza mawasiliano ya moja kwa moja na Newcastle katika jitihada za kufikia makubaliano ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.

Newcastle, Bayern Munich Waanza Mazungumzo ya Anthony GordonInaelezwa kuwa Newcastle kwa sasa inahitaji kiasi cha euro milioni 90 ili kumuachia Gordon, lakini Bayern Munich haipo tayari kulipa fedha hizo na inaamini dili hilo linaweza kukamilika kwa kiasi cha kati ya euro milioni 75 hadi 85 pamoja na bonasi mbalimbali.

Newcastle, Bayern Munich Waanza Mazungumzo ya Anthony Gordon“Bayern Munich na Newcastle wako kwenye mazungumzo ya klabu kwa klabu kuhusu Anthony Gordon,” ilieleza taarifa hiyo huku ikiongeza kuwa bado hakuna makubaliano rasmi yaliyofikiwa kati ya pande hizo mbili.

Newcastle, Bayern Munich Waanza Mazungumzo ya Anthony GordonMbali na Bayern Munich, klabu za Liverpool FC, Arsenal FC pamoja na FC Barcelona nazo zinafuatilia kwa karibu hali ya Gordon baada ya kufahamu kiwango cha fedha kinachohitajika ili kuipata saini ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa England.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.