Mchezaji wa Zamani wa Barcelona Xavi Hernandez akataa kazi ya kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Brazil itakayomfanya asaidie kujenga timu hiyo mpaka kombe la dunia la 2022 huku Qatar.

Jarida la AS la hispania liliandika kuwa Shirikisho la soka la Brazil limemfuata Xavi na kufanya mazungumzo naye kuhusu kuja kuwa msaidizi wa kocha mkuu wa timu hiyo ya taifa Tite kuelekea maandalizo ya mwisho mwisho ya kombe la dunia.

Xavi, ambaye anafundisha timu ya Al Sadd huku Qatar alikataa ofa hiyo huku akishangazwa na yeye kutakiwa na timu ya taifa ili akawe kocha wa timu hiyo. Hata hivyo chanzo cha habari kilidai kuwa yaliyokuwa ni mazungumzo ya awali na hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa na pande zote mbili.

Hivi karibuni Xavi aliongeza Mkataba wa kuendelea kusalia klabuni hapo mpaka 2023, huku akiisaidia timu ya Al Sadd kushinda taji la Qatar Domestic Leagu bila ya kupoteza hata mchezo mmoja. Hernandez alijiunga na klabu hii mwaka 2015 akiwa kama mchezaji baada ya kushinda makombe 17 akiwa na Barca, kabla ya kuwa kocha rasmi wa timu hiyo 2019.

Kuna tetesi mbalimbali zinazoeleza kuwa kocha huyu atarudi Barcelona na kuwa kocha wa timu hii, kufuatia hali ya sintofahamu juu ya hatima ya kocha wa Barcelona wa sasa Koeman ambaye amepotea kabisa kwenye radar za ubingwa wa LaLiga msimu huu baada ya kichapo cha juzi cha 2-1 dhidi ya Celta Vigo.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

Xavi, Xavi akataa ukocha kuelekea kombe la dunia 2022, MeridianbetBASHIRI SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa