Uongozi wa klabu Yanga umesema kuwa licha ya kupoteza mchezo wao jana dhidi ya Azam FC bado wana nafasi ya kufanya vizuri katika mechi zijazo na bado hawajakata tamaa.

Mechi hiyo iliyochezwa jana katika uwanja wa Mkapa, saa 2:15 usiku, kati ya Azam FC na Yanga ambapo Azam iliibuka mshindi wa bao 1-0.

Goli hilo la ushindi lilopachikwa na Prince Dube dakika ya 85 kwa shuti kali nje ya 18 lililomshinda mlinda mlango, Faroukh Shikalo na kuwafanya wapoteze mchezo huo wa mzunguko wa pili.

 

YangaOfisa Uhamasishaji wa Yanga Bw Antonio Nugaz, amesema kuwa ni matokeo mabaya ambayo wanayapata watayafanyia kazi.

Hakuna kukata tamaa. Tuendelee kupambana kwenye kila mchezo kwa kila namna ibakie matokeo ya mpira na bahati ya siku yenyewe.”

Azam FC imefikisha jumla ya pointi 54 ikiwa nafasi ya tatu huku Yanga ikibaki kuwa na pointi 57 nafasi ya pili kwenye msimamo. Kinara ni Simba mwenye pointi 58 baada ya kucheza mechi 24.


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

mini power roulette

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

CHEZA HAPA

11 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa