Baada ya mabosi wa Yanga kumtambulisha rasmi mrithi wa mikoba ya Cedric Kaze kwa mashabiki wao tayari ameanza kazi kwa ajili ya kukinoa kikosi hicho kuelekea kwenye mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.

Nasreddine Nabi ambaye ni raia wa Tunissia amepewa dili la mwaka mmoja na nusu kukinoa kikosi hicho ambacho kilikuwa mikononi mwa Juma Mwambusi aliyekuwa akikaimu nafasi ya Kaze iliyoachwa wazi tangu Machi 7, 2021.

Yanga - Nabi conference

Raia huyo wa Tunissia jana alianza kuwanoa nyota wa kikosi hicho wakiongozwa na kipa Faroukh Shikhalo, Ditram Nchimbi, Kibwana Shomari, Feisal Salum, Saido Ntibanzokiza kwa ajili ya mechi ya kesho ya ligi dhidi ya Azam FC.

Yanga ikiwa inaongoza ligi baada ya kucheza mechi 26 kesho Uwanja wa Mkapa inakazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Azam FC kwenye mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Yanga - Talking

Azam ipo nafasi ya tatu na pointi 51 inakutana na vinara wenye pointi 57 jambo ambalo litaongeza ushindani.

Kwenye mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Azam Complex, ubao ulisoma Azam 0-1 Yanga.

Nabi amesema kuwa anatambua wachezaji wake wapo imara na amewaambia kwamba wana kazi ya kuonyesha vitendo kwenye mechi zote.


MKWANJA MARIDHAWA NA KASINO YA 777 MEGA DELUXE

Nafasi nyingine kwaajili yako, kasino mpya yenye hadhi ya kipekee inayokupa kila sababu ya kuwa mshindi katika kasino za Meridianbet, anza siku yako na njia rahisi ya kutengeneza mkwanja.

yanga, YANGA: Kocha Mpya Ameanza Kazi Rasmi, Meridianbet

CHEZA HAPA

10 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa