Nahodha wa Yanga, Lamine Moro leo ameitwa na Uongozi wa juu wa Klabu ili kusikiliza shauri lake la Utovu wa nidhamu lililowasilishwa kwa Uongozi na Benchi la Ufundi.

Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, CPA. Haji Mfikirwa amesema, baada ya kupata malalamiko kutoka benchi la ufundi ni muhimu kusikiliza upande wa pili ili kutoa maamuzi ya haki kwa pande zote.
Yanga - LemineBenchi la Ufundi limelalamika, na kwa nafasi yao walichukua hatua za awali zilizoko kwenye Mamlaka yao, kwa kuwa wamelileta kwa Uongozi, sasa ni muhimu Sana tukamsikiliza mlalamikiwa kisha kutoa maamuzi kama klabu,” amesema CPA. Haji.

Amesema suala la Lamine ni la kinidhamu lililoanzia kwenye bechi la ufundi na halihusiani chochote na kuidai klabu na kwamba nyota huyo hana deni lolote analoidai klabu kwa mujibu wa makubaliano.

Lamine hadai chochote, hivyo taarifa za kwamba anaidai klabu ni za uzushi na zipuuzwe, suala lake limetokana na masuala ya benchi la ufundi, na tutalitolea taarifa baada ya kamati kukaa na kusikiliza,” amesema.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

yanga, YANGA: Lamine Hadai Chochote, MeridianbetBASHIRI SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa