Klabu ya Yanga SC imempitisha Eng Hersi Said kuwa mgombea pekee wa nafasi ya urais ambaye amepita bila kupingwa kutokana na kutokuwepo mgombea mwengine ambaye aliomba kugombea kiti cha urais.

Klabu ya Yanga imefungua kampeni kwa wagombea wa ngazi zote kupiga kampeni, ili kuweza kushawishi wanachama wa klabu hiyo. Upande wa urais ni Eng Hersi Said yeye yupo sehemu salama ambapo anasubiri kuapishwa.

Eng Hersi Said, Eng Hersi Said Rais Mpya wa Yanga Anayehitaji Kuapishwa, Meridianbet

Wanaowania nafasi ya makamu wa urais ni Arafat Haji na Suma Mwaitenda, huku nafasi za wajumbe wa kamati ya utendaji wakiwa 17 waliopitishwa.

Leo kwenye kikao na waandishi wa habari kwenye hotel ya Serena, Eng Hersi Said alikuwa akitoa sera zake na kumpigia kampeni mgombea wa nafasi ya makamu wa urais Arafat Haji.

Awali Eng Hersi alikuwa ni mtendaji wa kamati ya usajiri wa klabu ya Yanga pia Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM / Yanga SC.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa