Mshambuliaji mpya wa klabu ya Yanga Lazarious Kambole ameanza rasmi mazoezi kwenye kikosi hicho tayari kwa ajili ya kujiweka fiti kwenye michezo inayowakabili klabu hiyo msimu huu.

Kambole ambaye ni raia wa Zambia alisajiliwa na Yanga kwenye dirisha hili kubwa la usajili akitokea Kaizer Chiefs baada ya mkataba wake kumalizika.

YANGA,., Kambole Aanza Mazoezi Rasmi Yanga, Meridianbet

Tangu kuanza kwa msimu huu ambapo Yanga tayari imecheza mchezo mmoja wa ligi dhidi ya Polisi Tanzania nyota huyo hajacheza kutokana na kusumbuliwa na majeraha.

Akizungumzia hali ya kikosi kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Coastal Union, Kocha Mkuu wa Yanga, Nassredine Nabi amesema kuwa kikosi kimekamilisha maandalizi.

“Kikosi kimekamilisha maandalizi kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Coastal Union na tunaenda kupambana kwa ajili ya kuhakikisha tunapata matokeo.

“Kambole ameanza kufanya mazoezi leo asubuhi na timu lakini hatujamjumuisha kwenye mipango yetu ya mchezo wa kesho.

“Tofauti na Yacouba Songne ambaye ana majeraha ya muda mrefu wachezaji ambao watakosekana kwenye mchezo wa kesho ni Djigui Diarra na Salum Aboubakar ‘Sure Boy’.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa