KUREJEA kwa mshambuliaji Mzambia Lazarous Kambole kumemlazimu Kocha Mkuu wa timu ya Yanga Nasreddine Nabi kutengeneza kombinisheni mpya ya ushambuliaji hatari.

Mzambia huyo alikuwa nje ya uwanja kwa wiki mbili akiuguza maumivu ya misuli aliyoyapata kwenye pre-season walipocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo FC huko Avic Town.

Yanga, Kambole Arejea kwa Kishindo Yanga, Meridianbet

Mmoja wa mabosi wa timu hiyo, alisema kuwa mara baada ya Kambole kurejea uwanjani, kocha ameonekana akiijaribu kombinesheni yake na kiungo mshambuliaji raia wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki.

Bosi huyo alisema kuwa kocha huyo ameonekana kumchezesha Kambole namba 9 huku Aziz Ki nyuma yake 10 ambaye amempa jukumu la kumchezesha kwa mipira mizuri ya kufunga wakiwa mazoezini huko Avic Town.

“Tuna jumla ya washambuliaji watatu katika timu, ambao wote anakubali uwezo wao kutokana na umahiri mkubwa wa kufunga mabao walionao uwanjani.

“Hivyo basi anajaribu kutengeneza kombinesheni tofauti za ushambuliaji, mara kadhaa amekuwa akimchezesha Mayele, Makambo wote wakicheza namba 9 lakini nyuma yao anakuwepo Aziz Ki.

“Lakini juzi mara baada ya Kambole kurejea uwanjani na kufanya mazoezi ya pamoja na wenzake, ameonekana akimchezesha pamoja na Aziz Ki.

“Kwa maana ya Kambole kucheza namba 9 na Aziz Ki 10, kocha huyo anaitengeneza kombinesheni hiyo mpya ya ushambuliaji kwa lengo la kusuka kikosi imara ambacho hakitamtegemea mchezaji mmoja pekee katika timu,” alisema bosi huyo.

Nabi alizungumzia hilo kwa kusema: “Najaribu kutengeneza ushindani wa namba katika timu kwa kila mmoja kupambania namba ili aingie katika kikosi cha kwanza.

“Kama nilivyoongea awali, bado kikosi changu hakijakamilika kwa asilimia mia moja, hivyo najaribu kutengeneza timu itakayokuwa imara na kutengeneza mzunguko wa wachezaji kucheza kwa kupishana kwa lengo la wengine kupumzika, kwani tuna mashindano mengi msimu huu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa