Sentensi nzuri zaidi ambayo shabiki wa Yanga wanaweza kuisema zaidi ya ‘mmekwisha’ baada ya Kamati ya Sheria na Hadhi za wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kupitisha usajili wa winga wa DR Congo Tuisila Kisinda kucheza Yanga.

TFF, wametoa taarifa hiyo leo usiku ikieleza kuwa wamepitisha jina la Kisinda kwenye usajili baada ya Yanga kumuhamisha, straika Lazarous Kambole  na nafasi yake kuchukuliwa na Kisinda ili kutimiza idadi ya wachezaji 12.

Yanga, Kisinda Ruksa Kuitumikia Yanga, Meridianbet

Taarifa ambayo TFF waliitoa ilisema, awali Kamati hiyo ilizuia usajili wa Kisinda licha ya kuwa ulifanyika ndani ya dirisha la usajili kwa vile tayari Yanga ilikuwa na wachezaji 12 wa kigeni.

Taarifa hiyo ilisomeka hivi: “Kamati ya Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imepitisha usajili Wa Tuisila Kisinda kuichezea Yanga baada ya klabu hiyo kumhamisha mchezaji wake wa kigeni Lazarous Kambole.
 
“Awali kamati hiyo ilizuia usajili wa Kisinda licha ya kuwa ulifanyika ndani ya dirisha la usajili kwa vile tayari Yanga ilikuwa na wachezaji 12 wa kigeni.
 
“Licha ya changamoto hiyo, pia Kisinda aliombewa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ambayo tayari imepatikana.
 
“Hivyo kwa kumuhamisha Kambole imepata nafasi ya kumsajili Kisinda kama ilivyokuwa imeshauriwa huko nyuma. Kwa mujibu wa kanuni ya 62 (1) ya Ligi Kuu Toleo la 2022, klabu inaruhusiwa kusajili wachezaji wa kigeni wasiozidi 12.
 
“Kambole amejiunga na timu ya Wakiso Giants inayocheza Ligi Kuu Uganda na tayari TFF imetoa ITC.”


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa