Kamati ya maadili ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) limemfungia Ofisa mhamasishaji wa Yanga, Haji Manara kwa miaka miwili pamoja na faini ya Milioni 20 kwa kosa la kumtishia na kumdhalilisha Rais wa TFF, Wallace Karia.

Akizungumzia adhabu hiyo Katibu wa kamati ya maadili ya TFF, Walter Lungu amesema kuwa shauri hilo liliwasilishwa kwenye kamati hiyo baada ya mchezo wa kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

Manara, Manara Miaka Miwili Nje ya Soka na Faini ya Milioni 20, Meridianbet

“Shauri la maadili liliwasilishwa na kamati ilianza kupitia kuanzia Julai 11 mwaka huu, kwa makosa ya kumtishia na kumdhalilisha Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

“Matukio hayo aliyafanya kwenye mchezo wa fainali wa mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha alisikika akisema kuwa ‘Wewe unanifuata fuata sana na hii ni mara ya tatu huwezi kunifanya chochote.

“Katika kujitetea kwake Manara alisema kuwa si kweli na hakuzungumza hilo. Julai 20 kamati ilikutana tena kupitia shauri hilo huku Haji akiitwa kufika kwenye kikao cha kamati ambapo hakufika.

“Alipotafutwa kwenye simu haikupatikana na alipofuatwa ofisini kwake hakuwepo na waliokuwepo walisema anaumwa na alilazwa hospitali lakini wanasheria walipofuatilia waligundua ni vipimo vya kawaida.

“Kamati imejiridhisha kuwa haji ametenda makosa na adhabu yake ni kufungiwa miaka miwili pamoja na faini ya Mil 20 ambapo Adhabu hiyo itaanza kutekelezwa leo Julai 21.

“Endapo upande wa mlalamikaji na mlalamikiwa kwa yeyote anayetaka kukata rufaa ipo wazi.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa