KOCHA Mkuu wa Polisi Tanzania, Joslin Sharif amefunguka kuwa tayari ameongea na mabeki wake ili kuhakikisha hawafanyi makosa na kuadhibiwa na straika wa Yanga, Fiston Mayele. 

Mchezo huo wa ligi unatarajia kupigwa leo jumanne kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

Polisi Tanzania, Polisi Tanzania Wamuhofia Fiston Mayele, Meridianbet

Kocha Joslin amesema “Tunamshukuru Mungu kikosi kipo salama na morali ni kubwa kuelekea kwenye mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Yanga.

“Tunatambua umuhimu wa huo mchezo na tumeona wapinzani wetu wana kikosi kizuri lakini hata sisi tumewasajili wachezaji wazuri hivyo tuna imani wataenda kupambana. 

“Mayele ni mchezaji mzuri anajua kufunga ila ana miguu miwili kama wachezaji wetu hivyo wataenda kucheza kwa tahadhari. 

“Nimewafundisha mabeki wangu na kuwaambia kwamba wasifanye makosa yale ambayo yatasababisha kupoteza mchezo kama ule wa msimu uliopita hivyo nina imani wataenda kuyatekeleza.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa