Rais Hersi Said ameweka wazi kuwa mahitaji yao ni kuweza kuwa kwenye mwendelezo wa kuwa na rekodi bora kwa msimu wa 2022/23 kama walivyofanya msimu uliopita wa 2021/22.

Msimu wa 2021/22 Yanga iliweza kutwaa mataji matatu bila kupoteza mchezo kwenye mechi ambazo walicheza jambo ambalo linawafanya wajivunie rekodi hiyo.

Hersi Said, Rais Hersi Said Anaitaka Rekodi Bora Yanga, Meridianbet

Rais Hersi Said amesema: ”Kutwaa mataji matatu kwenye mechi za ushindani bila kupoteza mchezo hilo ni jambo kubwa na rekodi hiyo bora tunahitaji iweze kuendelea kwa msimu ujao pia wa 2022/23.

“Tunatambua kwamba haitakuwa kazi rahisi lakini kwa wachezaji waliopo kuna jambo ambalo tutafanya,fikiria tulianza na Ngao ya Jamii tukashinda kisha ikaja ligi na Kome la Shirikisho huku kote tumetwaa mataji hayo bila kufungwa ilikuwa ni kazi kubwa na ngumu,” alisema Said.

Mataji yote matatu Yanga ilitwaa mikononi mwa Simba ambayo ilikuwa inatetea Ngao ya Jamii,Kombe la Shirikisho na ligi.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa