Mabingwa wa Ligi kuu ya Tanzania ‘NBC Premier League’ Yanga SC imeonesha utofauti kwenye mapokezi na ushangiliaji ‘Trophy parade of honour’ baada ya kukabidhiwa rasmi kombe lao jijini Mbeya na kurudi nalo jijini Dar es Salaam.

Klabu ya Yanga imekuwa bingwa mara 28, huku mpaka sasa akiwa hajapoteza hata mchezo mmoja, na akiwa amebakiwa na mchezo mmoja ambao unatarajiwa kupigwa jijini Dar es salaam dhidi ya Mtibwa Sugar 29 June.

Yanga

Kilichovutia zaidi msimu huu ni jinsi walivyoamua kuonesha utofauti wa jinsi ya kushangilia ubingwa wao, walikodi gari la wazi lenye nafasi juu kutoka nchini Uganda, pia hamasa waliyoitoa kwa mashabiki wao ili kuweza kuhudhuria kwa wingi kutoka uwanja wa ndege hadi kwenye jengo lao lilipo mtaa wa Twiga Kariakoo.

Watu mbalimbali na taasisi kubwa za michezo Afrika zimeipongeza yanga kwa kufanya jambo ambalo ni nadra sana kutokea, hasa kwenye ukanda wa Afrika mashariki na kati ambapo mwandishi mkubwa Ebenezer aliwaponeza na kocha mkubwa kabisa Afrika Pitso Mosimane aliipongeza Yanga.

“Hongereni yanga. Afrika pia inaweza kusherekea kama timu za ulaya. Tunahitaji kuona hivi mara nyingi kwa sababu inaonesha upendo na hisia za mashabiki. Uzuri wa soka la Afrika.

Pitso Mosimane

Yanga imekuwa timu ya kwanza nchini Tanzania kupokewa na Water Salute.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa