Yanga Kazi Kazi Ndani ya Avic Town

KIKOSI cha Yanga chini ya Kocha Mkuu, Nassredine Nabi kinaendelea kujifua kwenye kijiji cha Avic Town, Kigamboni kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Azam pamoja na ule wa kwanza wa kimataifa.

Yanga inatarajia kumenyana na Azam FC Septemba 6 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar ukiwa ni mchezo wa mzunguko wa tatu wa ligi.

Kubwa zaidi kwa mashabiki wa kikosi hicho ni pamoja na kurejea kwa straika mpya ndani ya kikosi hicho Lazarious Kambole ambaye alikuwa anasumbuliwa na majeraha.

Wakati Yanga wakicheza mechi mbili za Ligi na ule wa Ngao ya jamii Kambole alikuwa nje ya kikosi kutokana na majeraha ambayo yalimuweka nje ya kikosi tangu asajiliwe akitokea Kaizer Chiefs.

Akizungumzia hali ya kambi yao, Meneja wa Yanga, Walter Harrison amesema kuwa “Timu inaendelea na mazoezi, wachezaji wana morali kubwa na kila mtu anatamani kupata nafasi ya kucheza na Habari nzuri ni kwamba kambole ameanza mazoezi na wenzake.”

Acha ujumbe